Kumbe Alivamiwa! Kisa Cha Nandy Kuvua Pete Ya Bill Nass Hiki Hapa

Nandy Azungumzia Kuvua Pete Ya Bill Nass

By  | Nov 20, 2020, 01:08 PM  | Relationships

Moja ya  habari inayoshika kwa kasi hapa mjini kwenye anga za burudani ni Nandy na Bill Nass na hivi karibuni uvumi umekuwa ukienea wa Nandy kuvua Pete ya Bill.

Akizungumza leo katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Nandy amefunguka kuwa hajawahi kukaa muda mrefu akiwa hajavaa pete ila watu hawakuwa wanaliangalia hilo.

“Sijawahi kukaa muda mrefu sijaivaa pete eti sababu kuna ugomvi au vinginevyo, inatokea labda usiku nimeivua, nimeamka asubuhi kuna emergency nikaondoka nikaisahau na hapo nikipiga picha unakuta mtu anahoji ” alisema Nandy.

Alisema, kwa sasa havai pete kwa sababu walikua Tanga kwenye masuala ya kampeni mashabiki wakamvua pete.

Nandy anafafanua kuwa, katika kuvutwa na mashabiki aling’olewa kucha na kuchukuliwa pete.

Kwa upande wake Bill Nass amefunguka kuwa, ana mpango wa kmnunulia Nandy pete nyingine kutokana na kwamba awali walivishana pete bila kuhusisha familia.

“Safari hii ntanunua pete nyingine na atavaa katika misingi mingine sahihi. Pete ile iliyoibiwa ilikua ni ya Sapraizi kwa hiyo haikuwa inafiti kwenye kidole”. Alifafanua Bill Nass

Read more