Ikulu Yampukutisha Kanye West Bil 6

Mbio za Ikulu Zampukutisha Mabilioni Kanye

By  | Nov 20, 2020, 01:09 PM  | Drama

Post main image
Mbio za urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Novemba 3, mwaka huu, zimesababisha rapa Kanye West atumie tena Dola za Marekani milioni 3 (zaidi ya Sh bil. 6 za Tanzania).

Kwa mujibu wa The Blast, Kanye ameshatumia jumla ya Dola milioni 9.76 ukipigia hesabu fedha zote alizomwaga kwenye kampeni tangu alipotangaza nia ya kushindana na rais kupimana ubavu muhula wake wa pili, Donald Trump.

Inafahamika kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zimetoka katika miradi yake kwani Tume ya Uchaguzi ya Marekani ilimpatia Dola 2,782 tu kwa ajili ya shughuli za kuisaka Ikulu, ikiwamo kufanya kampeni.

Kanye, ambaye wengi walimfahamu kuwa ni swahiba wa Trump, ameshapata uungwaji mkono katika majimbo 12 na ameendelea kuomba wananchi wa maeneo mengine wampitishe kuwania kiti hicho cha urais.

Read more